Facebook

Friday 29 August 2014

Eto'o atundika 'daluga' kimataifa


Mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto'o
ametangaza kustaafu soka la kimataifa. Eto'o,
33, ambaye ameifungia Cameroon magoli 54
alijiunga na Everton siku ya Jumanne. Hatocheza
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka
2015 nchini Morocco, iwapo Cameroon
watafuzu. Uamuzi huu umekuja baada ya
kutojumuishwa kwenye kikosi cha Volker Finke,
na unahodha kupewa Stephane Mbia. "Napenda
kuwaarifu kuwa nimefikia mwisho wa kucheza
soka la kimataifa." amesema kupitia ukurasa
wake wa Instagram.

0 comments:

Post a Comment