Facebook

Friday 29 August 2014

Giroud kukaa nje hadi Disemba kutokana na majeruhi.


Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud
hatocheza hadi mwisho wa Disemba baada ya
kufanyiwa upasuaji kutokana na jeraha la mguu.
Klabu hiyo ilipata matokeo ya vipimo vya pili
siku ya Alhamis, ambavyo vimethibitisha kuwa
mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa
amevunjika muundi goko wa kushoto (left tibia).
Giroud, 27, ambaye aliumia katika mchezo dhidi
ya Everton ambao ulimazilika kwa sare ya 2-2,
hatoweza kucheza kwa karibu miezi minne.
"Utaniuliza kama nitanunua mchezaji gani kuziba
pengo la Giroud. Kwa sasa, hakuna." amesema
boss wa Gunners Arsene Wenger.

0 comments:

Post a Comment