Facebook

Wednesday 27 August 2014

Di Maria asajiliwa rasmi Manchester United,aweka rekodi ya usajili Uingereza.

 
Manchester United imetangaza rasmi kuwa Angel Di Maria amekamilisha Uhamisho wake kwa Dau la Rekodi huko Uingereza la Pauni Milioni 59.7 akitokea Real Madrid ya Spain.
Mara baada ya kukamilisha taratibu za Uhamisho, Di Maria alisema: “Nina furaha kupita kifani kujiunga na Manchester United. Nilikuwa na raha kule Spain na Klabu nyingi zilinitaka lakini Man United ndio Klabu pekee ningeweza kuiacha Real Madrid ili kujiunga nayo. Louis van Gaal ni Kocha bora sana mwenye rekodi nzuri na nimevutiwa mno na dira na nia ya kila Mtu Klabuni hapa ili kuirudisha tena juu ambako ndiko inastahili kuwepo. Nani hamu kubwa kuanza kazi!”

Nae Meneja Louis van Gaal, akimkaribisha Di Maria, amesema: “Angel ni Kiungo wa kiwango cha Dunia lakini muhimu zaidi ni Mchezaji Kitimu. Hamna shaka kuhusu kipaji chake kisicho mfano. Ni mwepesi sana na hatari kwa Guu la Kushoto ambae anatisha Difensi yoyote ile. Uwezo wake kukokota Mpira na kuwakabili Mabeki na kuwadaa ni kitu cha furaha kukiangalia. Ni nyongeza safi sana kwa Timu!”

ANGEL DI MARIA –Wasifu:
KUZALIWA: Argentina, Februari 14 1988 (Miaka 26)
KLABU
2005-2007: Rosario Central (Mechi 35, Goli 6)
2007-2010: Benfica (76, 7)
2010-2014: Real Madrid (124, 22)
2008- Hadi sasa: Argentina (52, 10)

MATAJI:
Benfica: Primeira Liga, Taca da Liga (2)
Real Madrid: Champions League, Super Cup, La Liga, Copa del Rey (2), Supercopa de Espana
Argentina: Kombe la Dunia 2014 Mshindi wa Pili

Akiwa Man United, Di Maria anategemewa kuvaa Jezi Namba 7 ambayo kawaida huko nyuma Old Trafford huvaliwa na Magwiji na waliowahi kuivaa ni kina George Best, Eric Canton, Bryan Robson na David Beckham.
 
Di Maria aliwika huko Brazil alipoichezea Argentina kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Argentina kufika Fainali, lakini yeye hakucheza Fainali hiyo baada ya kuumia, na Argentina kufungwa Fainali hiyo na Germany Bao 1-0.
 
Di Maria alijiunga na Real Mwaka 2010 akitokea Benfica kwa Dau la Pauni Milioni 36 na kutwaa Ubingwa La Liga Mwaka 2012 na Walichukua Ubingwa wa Ligi mabingwa barani UlayaMsimu uliopita.
 
UINGEREZA-UHAMISHO WA BEI MBAYA:
-2011 Fernando Torres £50m Liverpool kwenda Chelsea
-2013 Mesut Ozil £42.4m Real Madrid kwenda Arsenal
-2011 Sergio Aguero £38m Atletico Madrid kwenda Manchester City
-2014 Juan Mata £37.1m Chelsea kwenda Manchester United
-2011 Andy Carroll £35m Newcastle kwenda Liverpool
-2014 Alexis Sanchez £35m Barcelona kwenda Arsenal

0 comments:

Post a Comment