Facebook

Wednesday 27 August 2014

Arsenal dimbani leo dhidi ya Beskitas;Kufuzu UEFA.

UCL-2014-15-LOGOLeo usiku Arsenal wanatinga Uwanjani kwao Emirates kurudiana na Klabu ya Uturuki Besiktas kwenye Mechi ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo yaLigi mabingwa barani Ulaya.
Wiki iliyopita huko Instanbul, Besiktas na Arsenal zilitoka 0-0 na Arsenal wanahitaji ushindi tu ili kufuzu kwani Sare yeyote ya Magoli itamaanisha Besiktas ndio wataingia hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ambayo droo yake itafanyika huko Monaco Siku ya Alhamisi.

Arsenal wanaingia kwenye Mechi hii bila ya Kiungo wao mahiri Aaron Ramsey ambae alipewa kadi nyekundu kwenye Mechi ya Kwanza huko Instanbul.
Pia Arsenal itamkosa Nahodha wao Mikel Arteta mwenye tatizo la Enka na vile vile kumkosa Straika wao Olivier Giroud ambae pia ameumia Enka.
Kukosekana kwa Giroud kunaweza kutoa namba kwa Chipukizi Yaya Sanogo au Lukas Podolski au hata Alexis Sanchez kuchezeshwa kama mshambuliaji au ikibidi, Arsene Wenger kumtumia Joel Campbell.
Wakati Besiktas wana Kikosi kamili na Straika wao Demba Ba yu tayari kurejea tena Jijini London kuitesa Arsenal kama alivyokuwa akifanya akiwa na Klabu yake ya zamani Chelsea, Klabu hiyo ya Uturuki itakuwa bila ya Meneja wao kutoka Croatia kwenye Benchi, Slaven Bilić, ambae alipewa Kadi Nyekundu katika Mechi ya Kwanza na hivyo kulazimika kukaa Jukwaani kwa Mechi hii.

0 comments:

Post a Comment