Facebook

Friday 29 August 2014

Di Maria afanya mazoezi na wachezaji wenzake kwa mara ya kwanza Manchester United

Mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa pesa iliyovunja rekodi katika soko la usajili Ligi Kuu ya Uingereza.Angel Di Maria,kwa mara ya kwanza ameanza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake huko Carrington AON Training Complex

Baada ya kusajiliwa kutoka Real Madrid,kwa kitita cha Paundi milion 59.7

Angel Di Maria ambaye amekuwa tumaini jipya kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kupoteza uelekeo katika mechi mbili za awali,amekabithiwa jezi namba 7 ambayo huvaliwa na magwiji katika klabu hiyo.

Kwa mara ya kwanza amejumuika na wenzake huku akionekana mwenye furaha na shauku ya kufanya makubwa katika klabu yake Mpya.

0 comments:

Post a Comment