Manchester
United wamekamilisha mazungumzo na Real Madrid na kukubaliana kulipa
Dau la Pauni Milioni 63.9 kumnunua Angel Di Maria ambayo ni rekodi kwa
Uingereza.
Leo hii Di Maria anatarajiwa kutua Jiji la Manchester kwa
mazungumzo ya mwisho na kujitayarisha kuikabili Burnley kwenye Mechi ya
Ligi huko Turf Moor Jumamosi ijayo.
Ada hii ya Uhamisho wa Di Maria itavunja rekodi ya Ununuzi wa Bei
ghali wa Fernando Torres ambayo Chelsea walilipa Pauni Milioni 50
kumnunua kutoka Liverpool Miaka Mitatu iliyopita.
Kwa mujibu wa Kituo cha TV cha Sky Sports, kupitia Mdadisi wao na
Mtaalam wa Masuala ya Soka ya Spain, Guillem Balague, Man United walitoa
Ofa ya Euro Milioni 60 na Real kutaka Euro Milioni 90 na hatimae
kukubaliana Euro Milioni 80 ambazo ni sawa na Pauni Milioni 63.9.
Mara baada ya Leo kutoka Sare 1-1 na Sunderland huko Stadium of
Light hapo jana, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, aliulizwa kuhusu Di Maria
na akajibu: “Klabu inapaswa kutangaza. Ikiwa mambo tayari tutakuja na
kuwaambia safi! Kwa sasa hatusemi lolote!”
Alipoulizwa moja kwa moja kama angependa kumsaini Di Maria, Van Gaal
alijibu ndiyo na kuongeza: “Pia nampenda Messi na nampenda Vidal na wapo
Wachezaji wengi Duniani nawapenda lakini wote hawawezi kuja Manchester
United!”
Huko Madrid hapo jana, Meneja wa Real Madrid, Carlo Ancelotti,
amethibitisha kuondoka kwa Angel Di Maria na kusema alikwenda Kituo cha
Mazoezi kuaaga wenzake.
Related Posts:
UHAMISHO WA WACHEZAJI ULIOKAMILIKA HADI HIVI SASA LIGI KUU UINGEREZA
KLABU za Ligi Kuu England zipo kwenye heka heka kubwa za kusajili
Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu mpya wa 2014/15 unaoanza Agosti 16
lakini Dirisha la Uhamisho litafungwa rasmi Septemba 1 Saa 7 Usiku kwa saa za Afr… Read More
Algeria yateua kocha mpya.
Christian Gourcuff ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Algeria siku ya
Jumamosi. Raia huyo wa Ufaransa anachukua nafasi ya Vahid Halilhodzic
aliyewapeleka Mbweha wa Jangwani katika raundi ya pili ya Kombe la Dunia
… Read More
Mourinho "Nimemaliza Usajili"
Boss wa Chelsea, Jose Mourinho amesema amemaliza kununua wachezaji
msimu huu baada ya kukamilisha usajili wa beki wa kushoto Filipe Luis
kutoka Atlètico Madrid. Luis ni mchezaji wa nne mpya kusajiliwa na Mouri… Read More
Nyota wa Nigeria asajiliwa West Brom.
West Brom wamemsajili mshambuliaji kutoka Nigeria Brown Ideye kwa kitita kinachodhaniwa kuwa pauni milioni 10.
West Brom wametangaza kuwasili kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
25 akitokea Dynamo Kiev siku y… Read More
Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya.
Fabio Borini, 23, anajiandaa kujiunga na Sunderland baada ya Liverpool
kukubali ada ya pauni milioni 14 (Sky Sports),
Baada ya kumchukua Filipe
Luis siku ya Ijumaa, Chelsea wanazungumza na Atlètico Madrid kuhusu
kums… Read More
0 comments:
Post a Comment