Matumaini ya Chelsea ya
Uingereza kufuzu katika fainali yao ya tatu ya kombe la mabingwa barani
Ulaya katika kipindi cha miaka sita iligonga mwamba uwanjani Stamford
Bridge baada ya Atletico Madrid ya Uhispania kutoka nyuma bao moja kwa
nunge katika kipindi cha kwanza na kuilaza the blues mabao matatu kwa
moja katika mechi ya mkondo wa pili.
Timu hizo zilikuwa zimetoka sare tasa katika mkondo wa kwanza huko Uhispania.Atletico walijitahidi kutafuta bao la ugenini ilikunusuru ari yao ya kuweka rekodi ya kufuzu kwenye fainali hizo na juhudi zao zilizaa matunda Adrian Lopez alipoisawazishia dakika moja kabla ya mapumziko.
Vijana hao wa Diego Simeoni hawakulegeza kamba, kipa wao Thibaut Courtois ambaye anaichezea Madrid kwa mkopo kutoka Chelsea alifanya kazi ya ziada kumzuia John Terry na David Luiz kufunga bao .
Wimbi baada ya wimbi la mashambulizi ya Atletico yalilegeza safu ya ulinzi ya Chelsea na kuzaa penalti baada ya ya mshambulizi wa camerooon Samuel Etoo kumwangusha Diego Costa .
Bao la ushindi lilifungwa na Adran Turan dakika kumi na mbili baadaye na kumhakikishia kocha Diego Simeone, fainali dhidi ya wapinzani wao kutoka mji wa Madrid Uhispania, Real.
Fainali hizo zitachezwa mjini Lisbon Ureno tarehe 21 Mei.
Ushindi huo umeipa Atletico tiketi yao ya kwanza ya fainali hiyo tangu mwaka wa 1972 .
Aidha hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo ambapo timu mbili kutoka mji mmoja zinachuana katika fainali.
Real Madrid ilijikatia tiketi ya fainali hizo baada ya kuwalaza mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich mabao 5-0
0 comments:
Post a Comment