Mlinzi wa Manchester
United Rio Ferdinand amesema ataondoka Old trafford msimu ujao baada ya
klabu hiyo kukataa kumuongezea muda kwenye kandarasi yake.
Kauli hiyo inamaanisha Ferdinand ambaye amefunga
mabao nane Old Trafford katika miaka 12 na kushiriki katika mechi 454
ataingia katika orodha ndefu ya wachezaji wakongwe mabalozi wa klabu
hiyo.Ferdinand alisema katika barua ya wazi kwa klabu hiyo kuwa angelipenda kuwaaaga mashabiki wake kwa njia bora zaidi lakini kutokana na ati ati hangeweza .
Hata hivyo amesema kuwa amefikiria sana kuhusu hatima yake na umewadia wakati wake kuwaaga.
Ferdinand aliwasili United Agosti 2002 kutokea klabu ya Leeds timu hiyo ilipokuwaikikabiliana na Hungary Zalaegerszeg katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Ameshinda mataji 6 ya ligi kuu ya premia mbali na mataji mawili ya nyumbani .
Manchester Utd pia ilishinda taji la klabu bingwa duniani mbali na taji la mabingwa barani Uropa.
0 comments:
Post a Comment