Facebook

Tuesday, 13 May 2014

Je timu ya mwisho duniani ni ipi ?

 
Nicky Salapu ,kipa aliyeshiriki mechi waliofungwa 31-0 na Australia
Mwaka wa 2001 timu ya Australia iliandikisha rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika kandanda ya kimataifa .
Australia ilifunga Samoa mabao 31 kwa nunge .
Mshambulizi wa Australia Archie Thompson,vilevile aliiingia katika daftari za kumbukumbu kama mfungaji mabao mengi zaidi katika mechi ya kimataifa alipofunga mabao 13.
Mvua hiyo ya mabao iliipelekea American Samoa kushuka ngazi na kujikita katika nafasi ya mwisho ya orodha ya mataifa yanayocheza kandanda ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 10.
Serikali,ya taifa hilo ilichukua jukumu la kumtafuta kocha mpya ilikuhakikisha timu hiyo inafuzu kwa kombe la dunia litakaloaanza mwezi ujao mjini Rio Brazil .
Kocha Mpya
Mjerumani Thomas Rongen ndiye aliyekabiliwa jukumu la kufufua hadhi ya kandanda katika kisiwa hicho mbali na kukomesha msururu wa matokeo duni na kushindwa katika kila mechi waliocheza ya kimataifa .
Kocha huyo alianza kwa kuwasaili wachezaji wliokuwepo katika mechi hiyo ya kihistoria huku akifahamu kuwa matamanio ya takriban wasamoa eflu 65 yalikuwa mabegani mwake .
Kocha mjerumani Thomas Rongen aliyeifufua timu ya Samoa
Aidha moyo wa wachezaji na motisha waliokuwa nao ilimshangaza kocha Rongen.
''Itakuwaje mtu anawania kuiwakilisha taifa lake katika kikosi ambacho kimeshindwa katika mechi zote ?''

Kiungo Jaiyah Saelua aliyeshiriki katika mechi hiyo alisema hata ingawa hawakuwa na viwango vya ushindani kama wachezaji wapinzani wao ilikuwa jambo la kujivunia kuvalia jezi la taifa.
Kila mtu alimshauri kocha huyo anayeishi marekani dhidi ya kuchukua wadhfa huo kwani ingemletea fedheha.
Hata mkewe alimzomea kuwa punguani endapo atachukua hatamu American Samoa.
Timu ya taifa ya Samoa
Lakini Mjerumani huyo alitua Samoa kwa kishindo na kuanza kazi na wachezaji waliokuwepo huko akiwemo mwanamke Jaiyah Saelua, aliyezaliwa kama mwanaume akiitwa Johnny,lakini maumbile yake yakabadilika na kuwa ya kike.
Kwa ufupi mwaka mmoja tangu hapo Novemba 2011, American Samoa ilisajili ushindi wake wa kwanza katika historia yake kwa kuandikisha ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tonga.
Ushindi huo ulikuwa wa kwanza baada ya kushindwa katika mechi 30 zilizochezwa katika kipindi cha miaka 20.
Kocha Thomas Rongen aliongoza timu hiyo kusherekea ni kama walioshinda kombe la dunia akisema kuwa hiyo kwa hakika ilikuwa ni historia .
Timu hiyo ilijizolea pointi 18 na ikaimarika hadi nafasi ya 197 kati ya mataifa 209 yanayoorodheshwa na shirikisho la soka duniani FIFA.
Nafasi ya mwisho 207 inashikiliwa kwa pamoja kati ya mataifa matatu Bhutan ,San Marino na visiwa vya Turks & Caicos

Related Posts:

  • Henderson afurahia Brendan Rodgers kubaki Liverpool.Kiungo Jordan Henderson amefurahia maamuzi ya uongozi kumbakisha kocha wa Liverpool Brendan Rodgers Kapteni huyo amesisitiza watamaliza msimu ujao kwa mafanikio na kuiletea heshima timu hiyo. Kocha Rodgers alikuwa na wakati m… Read More
  • Rais wa Afrika Kusini ahusishwa kashfa ya rushwa FIFA. Waziri wa michezo wa Afrika Kusini , Fikile Mbalula, sasa anasema rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki ndie aliyeruhusu ulipwaji wa fedha ,dola milioni 10 kwa FIFA , hela ambayo sasa inakumbwa na madai kwamba iliku… Read More
  • Mesut Ozil ajinyakulia tuzo Ujerumani.Mchezaji nyota wa Arsenal Mesut Ozil ameshinda tuzo ya balozi wa mpira wa Ujerumani 2015. Mesut Ozil ametangazwa kuwa balozi wa mpira wa Ujerumani mapema wiki hii.Tuzo hii hutolewa kwa watu wanofanya kazi za kuitolea.Ozil, a… Read More
  • Angel Di Maria "Nabaki old TraffordMchezaji raia wa Argentina Angel di Maria amethibitisha kubaki Manchester United msimu ujao. Pamoja na tetesi za kujiunga PSG kwa ada ya ya Euro milioni 60. Di Maria amefunga magoli manne na kutoa pasi za magoli 12 kwa mash… Read More
  • Xavi kuondoka Barca kwa heshima.Wakati Xavi Harnandez,35, anajiandaa na kustaafu rasmi baada ya kuitumikia Barcelona kwa miaka 17 ya maisha yake, swali je, atafanikiwa kuongeza kombe jingine hapo keshokutwa. Barcelona inashuka dimbani mjini Berlin, Uje… Read More

0 comments:

Post a Comment