Facebook

Monday, 12 May 2014

Gerrard:Liverpool itashinda taji kabla sijastaafu...




Nahodha wa Liverpool ya Uingereza Steven Gerrard amesema kuwa anaimani kuwa timu yake itashinda taji la ligi kuu ya Uingereza kabla hajastaafu kutoka katika kandanda.
Gerrad aliyasema hayo punde baada ya kuingoza timu yake kuilaza Newcastle United mabao mawili kwa moja katika siku ya mwisho ya mashindano msimu huu wa mwaka a 2013/2014
Licha ya ushindi huo Liverpool walimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Manchester City baada ya vijana wa Maunel Pellegrini kuilaza West Ham mabao mawili kwa nunge na kujihakikishia nafasi ya kwanza kwa jumla ya
alama 86 mbili zaidi ya Liverpool.
The Reds walikuwa wanahitaji City iakunguwae mikononi mwa West ham nao wasajili ushindi dhidi ya Newcastle iliwaipiku Manchester City kileleni mwa jedwali la ligi hiyo ya premia .
Kwa upande wao City walikuwa wanahitaji sare ya aina yeyote ile kujihakikishia taji la msimu huu.
Fauka ya hayo vijana wa Brendan Rodgers walisajili ushindi dhidi ya Newcastle iliyokuwa imesalia na wachezaji 9 uwanjani baada ya
Shola Ameobi na Paul Dummett kuoneshwa kadi nyekundu.
Baada ya Martin Skrtel kujifunga mwenyewe mapema katika kipindi cha kwanza ni Daniel Agger na Daniel Sturridge walioinua nyoyo za maelfu ya mashabiki waliokuwa wamefika Anfield.
Matokeo hayo hayakuwa na umuhimu wowote kwa maelfu ya mashabiki hao waliokuwa wameanza kuota kuwa Liverpool ingeshinda taji lao la kwanza katika kipindi cha miaka 24 .
Hata hivyo watajiliwaza kuwa, kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka wa 2009-10 Anfield itakuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la mabingwa barani Uropa msimu ujao.
Kwa upande wao Newcastle ilifunga msimu ikiwa katika nafasi ya 10.

0 comments:

Post a Comment