Jeshi la Thailand limetangaza
kuweka sheria za kijeshi katika juhudi za kurejesha utulivu wakati nchi
hiyo imekumbwa na mzozo wa kisiasa kwa muda.
Jeshi hilo pia limejitwika nguvu nyingi zaidi ili kuweza kutekeleza sheria hiyo.Hata hivyo Jeshi hilo, ambalo lilinyakua mamlaka mnamo mwaka wa 2006 limesema kuwa hatua yake sio mapinduzi bali ni hatua ya kudhibiti usalama wa taifa.
Sheria hiyo ya kijeshi imekuja kufuatia mvutano wa muda mrefu wa kisiasa kati ya serikali na upinzani.
Bado tuko uongozini
Mshauri mkuu wa masuala ya usalama kwa kaimu waziri mkuu, amesema kuwa hawakushauriwa juu ya hatua hiyo.Bwana Paradorn Pattanatabut amesisitiza kuwa kila kitu kinaendelea kama kawaida isipokuwa tu jeshi limedhibiti masuala yote ya usalama nchini humo.
Wanajeshi wameshika doria katika sehemu muhimu za nchi ikiwemo eneo ambapo wafuasi wa serikali wamekuwa wakiandamana nje kidogo ya mji mkuu Bangkok.
Tunataka demokrasia
Upinzani pia umekuwa ukisisitiza kuwa unataka uongozi wa nchi ukabidhiwe kwa bodi ya usimamizi ambayo haikuchaguliwa kidemokrasia, ambayo kwa sasa inasimamia masuala ya marekebisho ya katiba.
0 comments:
Post a Comment