Facebook

Wednesday, 21 May 2014

Mbu waanza kuvamia Uingereza


Mbu hawa wananofiwa kuanza kusababisha Malaria
Utafiti uliofanywa nchini Uingereza unaonyesha kuwa Mbu wameanza kuvamia maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.
Mabadiliko katika hewa ya mjini nchini Uingereza yameanza kutoa mazingira mazuri kwa Mbu kuishi, ikiwemo wale wenye uwezo wa kuambukiza ugonjwa wa Malaria na virusi vijulikanavyo kama 'West Nile virus'.
Utafiti unasema kuwa mazingira ya joto pamoja na vidimbwi vya maji katika nyumba za watu, yanawaleta Mbu karibu na watu.
Mbu wanaopatikana nchini Uingereza hawana uwezo wa kuambukiza maradhi yoyote, lakini wanasayansi hao wanasema kuwa jambo la wadudu hao kuzaana katika maeneo ya mjini linaongeza uwezo wa magonjwa kulipuka.
Wanasayansi hao hata hivyo wanakusanya data zaidi kuona ikiwa wengi wa wadudu pamoja na aina ya wadudu wenyewe inaweza kuchangia kwa vyovyote mlipuko wa maradhi au la, hasa katika maeneo ya mjini.
Viini vinavyosababisha Malaria
Kadhalika wanasayansi hao wanasema kuwa kutokana na ongezeko la viwango vya joto katika maeneo ya mjini,Mbu katika baadhi ya maeneo kama vile Kusini mwa Ulaya wameweza kusababisha magonjwa.
Pia wanasisitiza kwamba Magonjwa yamelipuka katika baadhi ya mataifa ya Ulaya kutokana na mabadiliko ya tabia ya Mbu.
Zaidi ya aina 30 ya Mmbu wamepatikana nchini Uingereza
"katika maeneo ya vijijini kuna Mmbu wengi zaidi kwa sababu ya mazingira tofauti tofauti, wengine wanapenda kuishi katika nyasi , wengine katika vidimbwi, na wengine katika mashimo,'' alisema mmoja wa wataalamu.
"lakini ukienda katika maeneo ya mijini , hakuna Mmbu wengi sana , labda utapa aina mbili au tatu ya Mmbu.
Daktari mmoja kwa jina Callaghan, alisema kuwa kulikuwa na visa vingi vya ugonjwa wa Malaria kila mwaka nchini Uingereza , wengi wanaokuwa wanarejea kutoka sehemu mbali mbali za dunia ambako ugonjwa Malaria unapatikana.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa mbalimbali kutoka pande zote dunia,utazipata hapa kwa wakati muafaka bila zengwe.

Related Posts:

  • Mahakama yazuia unywaji Pombe India. Mahakama ya rufaa nchini India imezuia mpango wa jimbo la Kerala Kusini mwa nchi hiyo kupiga marufuku pombe. Mamia ya wamiliki wa baa walikuwa wamepinga marufuku hiyo ambayo ingeanza kutekelezwa Ijumaa hii kwa kusema kuwa … Read More
  • Miaka 8 jela kwa jaribio la kutaka kumuua mkosoaji wa Rais wa RwandaWatu wanne - Watanzania wawili na Wanyarwanda wawili- waliokutwa na hatia ya kutaka kumuua mkosoaji wa Rais wa Rwanda Paul Kagame nchini Afrika Kusini wamehukumiwa kwenda jela kwa miaka minane kila mmoja. Mkuu wa zamani wa je… Read More
  • Binti alazimisha penzi kwa kumshikia Bastola mwanaume.Marekani: Binti (25) akamatwa kwa kosa la kumlazimisha kijana (33) kufanya naye mapenzi akiwa kamshikia bastoka kwenye gari lake baada ya kijana huyo kuomba lift. Inasemekana huyo binti alikuwa na mwanamke mwingine ambaye wal… Read More
  • Mahakama:Pistorius hakukusudia kuuaJaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp… Read More
  • Mchakato wa katiba kusitishwaKumekuwa na maoni tofauti kufuatia hatua ya kusitisha mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya nchini Tanzania. Katika kikao cha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na Viongozi wa vyama vya siasa nchini humo wamekubaliana kuwa ku… Read More

0 comments:

Post a Comment