Facebook

Monday, 12 May 2014

Kakobe:Ndoto Mpya inaitesa UKAWA


 Kama ilivyo kawaida kwa askofu Kakobe kuota ndoto mbalimbali kuhusu mambo yanayohusu mstakabali wa taifa letu. Askofu Kakobe ameota ndoto nyingine ambayo inawahusu UKAWA na harakati zao za kudai katiba ya wananchi.

Katika ndoto hiyo ya askofu Kakobe ambayo ameitoa leo katika ibada ya jumapili kwenye kanisa lake, amesema kuwa, kutokana na hali ya ubaguzi uliokithiri kwenye upinzani kupitia umoja wao huo wa UKAWA, haoni kama kutakuwa na mafanikio yoyote ya malengo ya wana UKAWA.

Askofu Kakobe katika kufafanua alieleza kwamba, viongozi wa UKAWA hasa mhe Mbowe hakuwa sahihi katika maamuzi yake ya kuwatenga waasisi wa upinzani nchini, akimaanisha mhe Mrema. Hivyo, kitendo hicho cha ubaguzi kitaondoa baraka iliyokuwa imepandikizwa awali kwenye umoja huo.

MAONI
Ni vyema sasa mhe Mbowe akachukua onyo hili na kufanya maamuzi sahihi ya kumuunganisha mhe Mrema na UKAWA. Kwa kuwa wote tunajua nguvu ya kiutabiri aliyonayo nabii Kakobe.

0 comments:

Post a Comment