Facebook

Monday, 12 May 2014

Video: Ni Unyama,Boko Haram wampiga mawe hadi kumuua msichana mmoja waliomteka Nigeria....angalia hapa....


Huu ni unyama ambao haupaswi kuvumiliwa uliofanywa na kikundi cha wanamgambo cha Boko Haram waliowateka Wasichana katika shule moja huko Nigeria.
Na inasemekana wamefanya unyama mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaua, kuwabaka na kuwafanyia vitendo vya kikatili wananchi mbalimbali wa Nigeria.
Ikiwa haitoshi hapo jana walituma video kaika mtandao wao ambayo chombo chetu kutokana na umakini tulikuwanao tulifanikiwa kuipata..ni katemimethsela.blogspot.com pekee ambapo unaweza kuangalia video hiyo hapo juu ...

Inayoonyesha ukatili uliofanywa na Boko Haram baada ya kumfukia msichana kwenye shimo kisha wakaacha kichwa kikiwa juu na kiwiliwili kufukiwa ardhini na wakaanza kumpiga mawe hadi kuaga dunia....

Kwa taarifa zilizotufikia punde ni kwamba Jeshi la Marekani limetuma askari wake waende kuwasaka wasichana hao waliotekwa na Boko Harama na waweze kukisambaratisha kikundi hicho kinachofanya unyama wa kutisha huko Nigeria na kusababisha majonzi makubwa kwa wazazi wa mabinti hao,Nigeria na Dunia kwa ujumla.....

              MUNGU IBARIKI NIGERIA....MUNGU IBARIKI AFRIKA

                   Photo: #RejesheniMabintiWetu

                                  #BRING BACK OUR GIRLS# 

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinajiri huko Nigeria baada ya kutumwa askari wa Marekani kwenda kuwakomboa wasichana waliotekwa na Boko Haram

0 comments:

Post a Comment