Juhudi za serikali dhidi ya kundi hilo hazijaonekana kuzaa matunda
Taarifa kutoka nchini Nigeria,
zinasema kuwa mamia ya watu waliuawa katika shambulizi lililofanywa na
kundi la wapiganaji wa Boko Haram katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon
siku ya Jumanne.
Kiongozi mmoja wa eneo
hilo, Ahmed Zanna, alisema kuwa washukiwa walivamia mji wa Gamboru
Ngala, katika jimbo la Borno, na kuwaua takriban watu 300.Inaarifiwa wapiganaji hao waliwafyatulia risasi watu kiholela katika soko kuu la eneo hilo.
Wandishi wanasema nchini Nigeria ilikuwa vigumu kupata taarifa hizo mapema kwa sababu ya changamoto ya mawasiliano katika jimbo hilo hasa kwa sababu eneo hilo liko mbali sana.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa walipata zaidi ya maiti miamoja kutokana na shambulizi hilo.
0 comments:
Post a Comment