Facebook

Sunday, 18 May 2014

Man Utd yamsaini kipa kinda kutoka Serbia


Vanja_Milinkovic-KIPA_MPYAMAN_UNITED 










MANCHESTER UNITED imekubaliana na Klabu ya Serbia, FK Vojovdina, ili kumsaini Kipa wao Chipukizi Vanja Milinkovic.
Milinkovic, Miaka 17, aling’ara mno akiidakia Serbia Mashindano ya Vijana ya UEFA U-17 na kuwafurahisha Man United baada ya kutofungwa Bao katika Mechi 3 kati ya 6.
Hata hivyo, Kipa huyo atabakia na Klabu yake FK Vojovdina kwa Msimu mmoja zaidi kabla hajahamia Old Trafford.
Wachezaji wengine waliowahi kuichezea Man United kutoka Nchini Serbia ni Nemanja Vidic na Zoran Tosic.
Milinkovic ni Mchezaji wa kwanza kuchukuliwa na Man United huku wakielekea kumthibitisha Meneja mpya wa Klabu hiyo, Louis van Gaal, ambae anatarajiwa kutangazwa Wiki ijayo na Wachezaji wengine wanaohusishwa kuhamia Old Trafford ni Mastaa waliojengeka kina Thomas Muller, Toni Kroos na Edinson Cavani.

LIVERPOOL YAWAWINDA XHERDAN SHAQIRI & RYAN BERTRAND!!
KUTOKA huko Liverpool, zipo habari kuwa Klabu hiyo inataka kumsaini Winga wa Bayern Munich Xherdan Shaqiri na Mchezaji wa Chelsea Ryan Bertrand ili kuimarisha Kikosi chao kwa ajili ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Mbali ya hao, pia Liverpool inatajwa kumsaka Beki wa Southampton Dejan Lovren.
Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, inadaiwa ana nia ya kukijenga Kikosi chake kwa kununua Wachezaji ambao wameshathibitisha ubora wao badala ya kuongeza idadi tu.
Shaqiri, mwenye Miaka 22, ni mmoja wa Wachezaji hao ambae ni nguzo ya Timu ya Taifa ya Switzerland aliejiunga na Bayern Mwaka 2012 kutoka FC Basel kwa Dau la Euro Milioni 11.6.
Hata hivyo, Mchezaji huyo wa Uswisi amekuwa hana namba ya kudumu na Bayern.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata taarifa mbalimbali zinazohusiana na usajili

0 comments:

Post a Comment