Facebook

Monday, 12 May 2014

Manchester City mabingwa Uingereza


Photo: CHAMPIONS 2014 #TOGETHER
Hatimaye Manchester City wamefanikiwa kunyakua ubingwa wa England katika siku ya mwisho ya Ligi Kuu, ambapo walikuwa wakihitaji pointi moja tu kutawazwa wafalme.
Vijana hao wa Manuel Pellegrini hawakufanya makosa walipoingia uwanjani nyumbani dhidi ya West Ham, kwani Samin Nasri na nahodha Vincent Kompany walihakikisha wanaipatia timu yao mabao, huku ngome ikihakikisha haivuji.
Wakati City wakipata ushindi huo, Liverpool waliokuwa wakiunyemelea ubingwa pia kwa kusubiri kuteleza kwa City, walianza vibaya baada ya Martin Skirttel kujifunga bao walipocheza dhidi ya Newcastle United na kuwafisha moyo washabiki dimbani Anfield.
Hata hivyo, Liverpool walizinduka baadaye, wakasawazisha kisha kufunga bao la ushindi lakini kwa kuzingatia matokeo ya City, Liver walishindwa kutimiza ndoto ya kutwaa ubingwa huo ambao waliupoteza tangu 1990.
City walikuwa wakipewa nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa huo, hasa baada ya Liverpool kuteleza hivi karibuni kwa kukubali kichapo kutoka kwa Chelsea, kabla ya mechi iliyopita kwenda sare ya 3-3 na Crystal Palace katika mchezo ambao vijana wa Brendan Rodgers walikuwa wanaongoza kwa mabao matatu kwa bila.
Nafasi ya tatu imekwenda kwa Chelsea ambao walianza vibaya mechi yao ya mwisho dhidi ya Cardiff kwa kutangulia kufungwa, lakini walisawazisha na kuongeza bao la ushindi katika kulindwa heshima yao. Nafasi ya nne imeshikwa na Arsenal waliowalaza Norwich 2-0.
Timu hizo nne ndizo zimeingia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) wakati Everton waliowafunga Hull mabao 2-0 na Tottenham Hotspur waliowakandika Aston Villa 3-0 wamefuzu kucheza Ligi ya Europa.
Manchester United wamemaliza msimu kwa sare ya 1-1 na Southampton.
Swansea waliwakung’uta Sunderland 3-1, West Bromwich Albion wakalala 2-1 kwa Stoke na Fulham wakatoka 2-2 na Crystal Palace.Norwich wameungana na Cardiff na Fulham kushuka daraja.
Photo: CHAMPIONS 2014 REACTIONS: Exclusive CityTV interviews with the players following today's Premier League triumph.

YAYA TOURE: http://manc.it/1grGylP
VINCENT KOMPANY: http://manc.it/1fZJqeN 
JAMES MILNER: http://manc.it/1grIHxS 
JESUS NAVAS: http://manc.it/1fZKXkTPhoto: CHAMPIONS 2014 REACTIONS: Exclusive CityTV interviews with the players following today's Premier League triumph.

JAVI GARCIA: http://manc.it/1grutgh
PABLO ZABALETA: http://manc.it/1gruErZ
EDIN DZEKO: http://manc.it/1grwtFm
FERNANDINHO:  http://manc.it/1grx3mBPhoto: CHAMPIONS 2014 REACTIONS: Exclusive CityTV interviews with the players following today's Premier League triumph.

ALVARO NEGREDO: http://manc.it/1gryotz 
JOLEON LESCOTT: http://manc.it/1grCamT
ALEKS KOLAROV: http://manc.it/1fZIGq3 
COSTEL PANTILIMON: http://manc.it/1grFsqa20140511-183236.jpg

Related Posts:

  • LUIS VAN GAAL "LAZIMA MUWEZE KUZUNGUMZA KIINGEREZA VIZURI"-Hayo ni maneno aliyo yazungumza Manager wa Man United LOUIS VAN GAAL akiwataka wachezaji wake wapya alio wasajili katika dirisha lililofungwa juzi waweze kuzungumza kiingereza vizuri ili iweze kuwasaidia vizuri katika kazi y… Read More
  • Clash of the Titans...Chelsea Vs Manchester CityUsithubutu kunywa uji wa mgonjwa...Wala mtoto hatotumwa dukani majira ya saa 12:00 Jion kwa masaa ya Afrika Mashariki mtanange kati ya Vijana wa Darajani,The Blues almaarufu kama Chelsea watakapopambana na The Citizen,Manches… Read More
  • RATIBA YA MECHI LIGI KUU YA UINGEREZA .BantuTz SPORTS RATIBA YA MECHI LIGI KUU YA UINGEREZA LEO HII 14:45 Liverpool vs Everton 17:00 Chelsea vs Aston Villa 17:00 Crystal Palace vs Leicester City 17:00 Hull City vs Manchester City 17:00 Manchester United vs West… Read More
  • Mourinho amponda Lampard. Mouringo akimuongelea Lampard baada ya kufunga bao lililopelekea matokeo dhidi ya City kua 1-1. 'Alipoamua kujiunga na wapinzani wetu tunaochuana nao kuwania ubingwa, hadithi za mapenzi zikaisha. Amefanya kazi yake (kufunga)… Read More
  • Yanga yaanza kwa Kipigo,Azam yaangua Kicheko Ligi Kuu Tanzania Bara.Dar es Salaam Young Africans imeianza ligi kuu kwa kichapo baada ya kufungwa 2-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri. Magoli ya Mtibwa yalifungwa na Musa Hassan Mgosi katika dakika ya 16 baada ya kupok… Read More

0 comments:

Post a Comment