Akipiga stori na mwandishi wetu, Natasha alisema tangu Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani, hajawahi kuugua hata homa lakini kwa mara ya kwanza mwaka huu homa ya dengu imemlaza.
“Nilianza kusikia baridi kali sana kisha nikawa naishiwa nguvu na mishipa inakakamaa, nilihisi naaga dunia kiukweli lakini niliwahi kwenda hospitali, nimepata tiba, nimeruhusiwa na ninaendelea vizuri,” alisema Natasha.
Miongoni mwa mastaa ambao wameumwa ugonjwa huo ambao hauna tiba ya moja kwa moja ni Rehema Chalamila ‘Ray C’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na Miss Afrika Mashariki namba 2, 2008, Aneth John.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot,com kujua afya za wasanii mbalimbali waliokumbwa na ugonjwa wa dengue
0 comments:
Post a Comment