Mama mmoja nchini Marekani, amejifungua mapacha waliozaliwa wakiwa wameshikana mikono.
Watoto hao pia walikuwa wanapumua bila usaidizi wowote walipotolewa kutoka katika mashine yenye hewa ya Oxygen."Tayari ni marafiki ,’’ alisema mama yao Sarah Thistlethwaite.
Walizaliwa Ijumaa katika jimbo la Ohio, wakiwa wameshikana mikono.
Inaarifiwa ni mama mmoja tu kati ya akina mama elfu kumi mwenye uwezo wa kujifungua mapacha wa aina hiyo.
Bi Thistlewaite, mwenye umri wa miaka 32,alilazimika kupumzika kwa wiki kadhaa kabla ya kujifungua kwani mapacha wanaozaliwa wakiwa wameshikana mikoni ni hali nadra ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya watoto hao kabla ya kuzaliwa.
Mama huyo alisema kupokea watoto wake ilikuwa zawadi tosha kwake wakati huu wa kusherehekea siku ya akina mama duniani.
0 comments:
Post a Comment