Facebook

Thursday, 15 May 2014

Mwanahabari wa Tanzania apata tuzo

Albino Tanzania
Albino akisuka mkeka, Tanzania
Mwandishi wa habari wa Tanzania Vicky Ntetema ameshinda tuzo ya kimataifa kutokana na ripoti zake kuhusu mauaji ya albino zilizotangazwa kwenye shirika la habari la BBC.
Wakfu wa kimataifa wa waandishi wa habari wa wanawake imempa tuzo ya ujasiri ya uandishi wa habari kwa uchunguzi wake.
"Sikutarajia lakini si kwamba nina furaha" Bi Ntetema  alisema kwamba mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne aliuliwa hivi karibuni.
Sikutarajia lakini si kwamba nina furaha
Vicky Ntetema
Baadhi ya watu wenye imani za kichawi wanasema dawa zinazotengenezwa na viungo vya mwili vya albino vinaweza kumletea mtu bahati na utajiri.
Takriban maalbino 53 wameuawa Tanzania katika miaka ya hivi karibuni, pamoja na wengine wengi katika nchi jirani ya Burundi.
Bi Ntetema amelazimika kukimbia nchini mwake mara mbili kutokana na ripoti hizo.

Amesema, "Siwezi kuwa na furaha wakati kumetokea mashambulio saba tangu tarehe 8 Februari baada ya kuwepo na utulivu tangu Oktoba mwaka jana."

Vicky Ntetema
Vicky Ntetema
"Nina wasiwasi kwamba huu ni mwaka wa uchaguzi na watu wenye imani za kichawi wanasema wanasiasa hutumia viungo hivyo kuhakikisha wanashinda."
Amesema pia kwamba maalbino ndio mashujaa halisi, hasa wale waliokatwa viungo vyao au wanawake waliokimbiwa na waume zao kutokana na kuzaa maalbino.
Bi Ntetema, mwenye umri wa miaka 51, ambaye kwa sasa anafanya kazi kwenye shirika la kutetea haki za binadamu, Under The Same Sun amesema, "Hao ndio mashujaa wa kweli."
Takriban maalbino 17,000 wanaishi kwa hofu nchini Tanzania, hasa vijijini kaskazini magharibi mwa nchi hiyo penye kufanyika mauaji mengi ya albino.

0 comments:

Post a Comment