Facebook

Friday, 16 May 2014

Sheikh Issa Ponda Arudishwa tena Rumande........

Kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ameendelea kusota rumande baada ya kesi yake kuahirishwa kwa mara nyingine kwa kuwa jalada la kesi yake, halijarudi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam lilikoitishwa kwa ajili ya mapitio.

Kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Morogoro mwaka jana, iko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mary Moyo na imekuwa ikitajwa kwa zaidi ya miezi sita, huku Sheikh Ponda akiendelea kusota rumande baada ya kunyimwa dhamana.

0 comments:

Post a Comment