Kocha wa timu ya taifa ya Brazil
Luiz Felipe Scolari,anatarajiwa kuchunguzwa na polisi kulingana na
taarifa kutoka ncini Portugal licha ya kocha huyo kukanusha madai kuwa
alikwepa kulipa kodi.
Bwana Scolari alikuwa kocha wa timu ya taifa ya
Portugal kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2008. Madai hayo yanaonekana
kuhusishwa na wakati wake alipokuwa nchini humo.Madai hayo yanakuja mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa kombe la dunia nchini Brazil.
Mwanasheria mkuu nchini Portugal amethibitisha taarifa za kuchunguzwa kwa Scolari, ingawa hakutoa taarifa zozote.
''Ninajiamini mimi mwenyewe sijafanya uhalifu wowote na nimekuwa nikitangaza mapato yangu. Ikiwa kuna jambo lolote ambalo haliko sawa , sio makosa yangu,'' alisema Scolari.
0 comments:
Post a Comment