Leo Bungeni:Mwigulu Amesema anachofanya Lissu ni jitihada zake za
kuwafitinisha Wazanzibari baada ya kushindwa kuwachonganisha Watanzania
Bara. Anasema kuwa wakati mwingina anaona aibu kujitambulisha kuwa
anatoka Singida kutokana na matendo ya Tundu Lissu. Anasema kuwa Lissu
ameongea mambo mengi ambayo hana takwimu wala hakika yake. Anawashangaa
Wazanzibari kwa kufurahia hotuba ya Lissu huku wanajua kuwa anafanya
jitihada za kuwagombanisha. Anasema kuwa mambo yakiharibika watakaoumia
ni Wazanzibari huku Lissu akifurahia kwake Singida.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua atakachojibu Tundu Lissu baada ya kauli hii ya Mwigulu Nchemba
0 comments:
Post a Comment