Serikali imetakiwa kutoa maelezo bungeni, kuhusu sababu za kuuawa kwa
waasisi sita wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wanaodaiwa kuzikwa
katika handaki moja Zanzibar.
Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Makadirio
ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), msemaji
wake, Tundu Lissu aliitaka Serikali kueleza waasisi hao walifanya makosa
gani.
Aliwataja waasisi hao kuwa ni Abdallah Kassim Hanga aliyekuwa Waziri
Mkuu, Abdulaziz Twala aliyekuwa Waziri wa Fedha na Saleh Akida aliyekuwa
Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na viongozi waandamizi wa Serikali ya
Mapinduzi, Othman Shariff, Mdungi Ussi na Jaha Ubwa ambao alisema
waliuawa na kuzikwa handaki moja eneo la Kama, Zanzibar.
Lissu alisema hayo huku akinukuu kitabu cha ‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri
Uhuru’ kilichoandikwa na Harith Ghassany alichosema kilionyesha jinsi
viongozi hao walivyouawa na kuzikwa katika kaburi moja.
“Sisi wa kizazi cha Muungano tunataka kujua ukweli juu ya makosa
waliyoyafanya hawa waasisi wa Muungano hadi wakauawa na kuzikwa katika
kaburi au handaki moja,” alisema Lissu huku wabunge wakiwa kimya
kumsikiliza.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kitakachoendelea kuhusiana na sakata hilo
0 comments:
Post a Comment