Maafisa nchini Cameroon wanasema kuwa kumekuwa na shambulizi katika kiwanda kimoja cha raia wa Uchina kazkazini mwa taifa hilo.
Ubalozi wa Uchina nchini Cameroon umesema kuwa
takriban watu kumi wametoweka huku mtu mmoja akijeruhiwa katika kile
ilichoelezea kama shambulizi kutoka kwa watu wasiojulikana.Kisa hicho kimetokea karibu na mpaka wa kazkazini mashariki mwa Nigeria ambayo ndio ngome kuu ya kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Wanamgambo hao wamefanya mashambulizi kadhaa nchini Cameroon .
Mwaka uliopita waliiteka nyara familia moja ya Ufaransa kabla ya kuiwachilia huru baada ya miezi miwili.
0 comments:
Post a Comment