Ajali mbaya ya gari imetokea muda si mrefu maeneo ya Chuo Kikuu cha Ardhi katika barabara inayoelekea Makongo karibu na hostel za wasichana (Low Cot).
Baada ya gari ndogo aina ya Toyota Vits iliyokuwa imebeba jumla watu 7, dereva na wasichana sita baadhi yao walikuwa wanatokea Chuo hicho.
Gari hiyo ilipata ajali baada ya dereva wa gari hiyo kutokujua na kufuata kanuni za barabarani kugeuzia gari barabarani na alipokuwa anajaribu kuingia barabarani ghafla gari aina ya Landcruiser VX iliyokuwa katika mwendo wa kasi kufunga breki ghafla lakini kwa bahati mbaya iliigonga gari ile ndogo ambayo tayari ilikuwa inataka kuingia barabarani.
Shuhuda wa ajali hiyo ambao ni wanafunzi mwaka wa kwanza katika Chuo hicho ambao hawakupenda kutajwa majina yao wanaeleza kuwa dereva huyo alikuwa na makosa baada ya kuingiza gari barabarani kinyume na sheria na taratibu za barabaranno.
Lakini cha kustaajabisha baada ya kutokea kwa ajali hiyo wasichana waliokuwa wamefuatwa na jamaa (dereva) huyo waliamua kushuka ghafla katika gari hiyo iliyokuwa imeharibika vibaya na kukodi bajaji kisha wakaondoka eneo la tukio na kumuacha dereva huyo akiomba msaada kwa watu baki,huku wasichana hao wakiendelea na ratiba zao za kujirusha kama zilivyokuwa zimepangwa....
Bahati nzuri katika ajali hiyo hakuna mtu yeyote aliyeumia lakini gari hiyo imeharibika vibaya hadi imeshindikana kuondoka katika eneo hilo.
Gari hiyo aina ya Toyota Vits ikiwa imeharibika vibaya baada ya kugongwa sehemu ya ubavuni na kidogo sehemu ya mbele
Gari hiyo inavyoonekana baada ya kugongwa vibaya
Mwanafunzi wa Chuo akitoa msaada kwa kutoa bati lililokuwa limenasa kwenye tairi la gari hiyo baada ya kutokea kwa ajali.
Gari hiyo aina ya Toyota Vits baada ya kuvutwa kutoka katika usawa wa barabara na kusogezwa pembeni ili utaratibu mwingine kufuatwa
Gari hiyo inavyoonekana kwa pembeni baada ya tukio hilo
Mwanafunzi
wa mwaka wa kwanza katika Chuo hicho akitoa msaada wa kuisukuma gari
hiyo ndogo iliyokuwa imeharibika vibaya baada ya kugongwa
Tabia
iliyoonyeshwa na wasichana hao sio nzuri na si ya kiungwana kwa
kushindwa kumuonyesha upendo na kumsaidia rafiki yao ambaye alikuwa
dereva wa gari ile.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora
zaidi.
0 comments:
Post a Comment