Ecuador ilitoka nyuma na kubana
Honduras mabao (2-1), katika mchuano wa kundi E, wa kombe la dunia
uliochezwa katika uwanja wa Arena da Baixada huko Curitiba.
Equador ilikua imeshindwa mabao 2-1 na Uswisi, katika mechi yao ya kwanza.Carlo Costly, ndiye aliyezima kiu hiyo ya miaka mingi baada ya dakika 31.
Wachezaji wa Equador walishindwa kuudhibiti mpira naye Costly akachukua nafasi hiyo baada ya kupata mpira kisha kuutia wavuni.
Honduras ilikua imecheza dakika 510, za soka bila kupata bao lolote.
Bao lao la mwisho katika kombe la dunia lilikua katika mechi yao ya pili, ya michuano ya mwaka 1982, walipotoka sare ya 1-1 na timu ya Ireland Kaskazini.
Dakika tatu baadaye, Ecuador ilisawazisha kupitia kwa mshambulizi Enner Valencia, aliyepewa pasi safi na mchezaji Juan Paredes.
Pasi hiyo iliipenyeza ngome ya ulinzi ya Honduras na kumpata Valencia aliyefunga bao hilo la kusawazisha.
Mnamo dakika ya 65, mchezaji Valencia tena aliupata wavu wa Honduras.
Walter Ayovi aliupiga mpira wa adhabu ambao ulimpata Valencia kwa kichwa naye akaugonga ukampita mlinda lango, Noel Valladares wa Honduras na kuingia kwenye wavu.
Valencia sasa ana mabao matatu katika kombe hili la dunia.
Awali, Honduras ilitoa tetesi baada ya bao walilolifunga kukataliwa na refa kwa madai ya kuotea kwenye lango la Ecuador.
Ushindi huo unawaweka Ecuador katika nafasi ya tatu na Uswisi katika kundi lao hata ingawa Ecuador ina mabao mengi zaidi.
Honduras pia bado ina matumaini kidogo ya kuendelea katika raundi ya pili.
Hili litategemea ikiwa wataishinda timu ya Uswisi Juma lijalo huko Manaus na kutumaini kuwa matokeo ya mechi hiyo nyingine baina ya Ufaransa na Ecuador huko MaracanĂ£, Rio de Janeiro, yatawaendea vyema .
0 comments:
Post a Comment