Facebook

Wednesday, 11 June 2014

Breaking News:Mwanza yachafuka,wamachinga wapambana na Jeshi la Polisi...

 
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka  mkoani Mwanza ni kwamba  kumetokea machafuko makubwa sana baada ya Jeshi la Polisi kupambana na Wamachinga.
   Ilikuwa ni mida ya asubuhi ambapo Jeshi la polisi lilikuwa limeshatoa tamko kwa wamachinga wanatakiwa kuondoka maeneo ya Stndi ya Tanganyika na Mtaa wa Makoroboi na kutofanya biashara katika maeneo hayo na kandokando mwa barabara katika jiji hilo linaloongoza kwa usafi nchini.
Wamachinga walipingana na tamko hilo na kuamua kugoma kuondoka maeneo yao ya kufanyia kazi hususan maeneo ya Tanganyika standi na Mtaa wa Makoroboi.Baada ya kugoma waendesha bodaboda nao wakaamua kuingilia kati huku wao wakiwaunga mkono wamachinga.
    Baada ya mgomo huo askari wa Jeshi la Polisi mkoani mwanza waliamua kwenda kuwatawanya wamachinga na waendesha bodaboda ndipo vurugu zilizpoanza kwani wamachinga walianza kuwarushia polisi mawe,miti,vipande vya kokoto na vyuma chakavu.

   Vilevile wamachinja walienda hadi eneo yalipo makao makuu ya manispaa ya Jiji la mwanza na kulichoma moto gari la manispaa.
   Kutokana na vurugu hizo jeshi la Polisi liliongezewa nguvu na Kikosi maalum cha kutuliza ghasia (FFU) ambao wao waliwatawanya wamachinga na Waendesha Bodaboda kwa kutumia mabomu ya machozi.

Huku baadhi ya wamachinga wakikamatwa na kupewa kipigo kikali.  
  Baada ya kikosi maalum cha kutuliza ghasia kufika eneo hilo wamachinga waliamua kukimbilia sehemu mablimbali hasa milimani na Ziwani.
  
 Kikosi maalum cha kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa wanawasili eneo la tukio-Stand ya Tanganyika
 
 Kikosi maalum cha kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa wanawasili eneo la tukio-Stand ya Tanganyika
Mtaa wa Makoroboi  ukiwa tulivu baada ya kuwasili kwa kikosi maalum cha kutuliza Ghasia (FFU) huku wamachinga wakiwa wamekimbia eneo hilo. 
Mmachinga mmoja ambaye kamera yetu ilimnasa akiwa amekimbilia ziwani kuhofia kukamatwa na kupewa kipigo kikali kwa askari.
Wamachinga wakiwa wametanda katika maeneo yao ya kufanyia biashara wakiwa wamekaidi tamko la Serikali la kuwataka kuhama katika maeneo yao ya kufanyia biashara. 

Baada ya kikosi cha kutuliza Ghasia kufika maeneo hayo na kurusha mabomu ya machozi wametoa tamko kwamba wamachinga waache fujo la sivyo watachukuliwa hatua kali wale wote watakao kamatwa kwa kiuka tamko hilo.

Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com...

0 comments:

Post a Comment