Zifuatazo ni baadhi ya picha kutoka Kigoma katika mazishi ya Bi
Shida Salum, mama mzazi wa Zitto Kabwe. Bi Shida alifariki Jumapili
asubuhi katika hospitali ya AMI jijini Dar Es Salaam baada ya kuugua kwa
muda mrefu.
Jeneza
lenye mwili wa marehemu Shida Salum likiwasili nyumbani kwa familia kwa
ajili ya shughuli za mazishi.
Mbunge
wa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akiwa na wabunge wenzie na
baadhi ya wazee wa Kigoma kwenye maandalizi ya mazishi ya mama yake
mzazi Bi Shida Salum aliyefariki Juni 1 katika hospitali ya AMI jijini
Dar Es Salaam.
Zitto Kabwe (mwenye kanzu nyeusi) akipewa pole na wageni waliofika kumfariji katika msiba wa mama mzazi.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakionekana kuumizwa na kifo cha Bi Shida Salum, mama yake Zitto Kabwe.
Kiongozi wa kidini akitoa mawaidha mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Bi Shida Salum, mjini Kigoma.
Umati
wa wakazi wa Kigoma wakisindikiza jeneza lenye mwili wa marehemu Shida
Salum (halionekani pichani) kwenda makaburini, Jumatatu mchana.
Tuko
katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma
zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi
0 comments:
Post a Comment