Rais Vladimir
Putin wa Urusi ameviweka vikosi vyake vilivyoko nchini humo katika hali
ya “tahadhari kamili ya vita” na kuwaamuru wanajeshi 65,000 katika eneo
hilo kufanya luteka za kijeshi za wiki moja kuwa tayari kwa vita.
Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu,
amesema mazoezi hayo ya kijeshi ya angani na ardhini katika maeneo ya
milima ya Volga na Ural yatafanyika kuanzia Jumamosi Juni 21 hadi Juni
28.
Jumuiya ya Kujihami ya NATO imesema mapema
wiki hii kwamba Urusi imerudia tena kurundika wanajeshi wake kwenye
mpaka na Ukraine ambapo waasi wanaotaka kujitenga wamekuwa wakipambana
na vikosi vya serikali kwa wiki kadhaa katika mzozo uliogharimu maisha
ya watu 300 na kuwapotezea makaazi wengine 34,000.
Kusitisha uhasama
Hatua hizo za kijeshi zinakuja siku moja
baada ya Rais Petro Poroshenko wa Ukraine kutangaza wiki moja ya
usitishaji wa mapigano na waasi wanaoiunga mkono Urusi mashariki ya nchi
hiyo ikiwa ni sehemu ya mpango wa amani wa vipengele vinne ambao pia
unajumuisha msamaha na ahadi ya kufanyika kwa marekebisho ya katiba.
Serikali ya Urusi imeishutumu mpango huo wa
Poroshenko kuwa ni “amri” ambao hautopelekea kupatikana kwa ufumbuzi
wowote ule na waasi wameukataa wito wake wa kuwataka wasalimishe silaha
zao.
0 comments:
Post a Comment