RAIS
wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo amesema kikosi cha sasa cha klabu
hii kitakumbukwa daima baada ya kuipiga chini Barcelona na kutwaa
ubingwa wa kwanza wa La Liga ndani ya miaka 18.
Vijana hao wa Diego Simeone walionekana kuwa hatarini kupoteza ubingwa mbele ya Barcelona siku ya jumamosi baada ya Wakatalunya kufunga bao la kuongoza kipindi cha kwanza, lakini kipindi cha pili, Diego Godin alisawazisha na kuwapa Atletico ubingwa.
Kufuatia kubeba ndoo ya La Liga, sasa Atletico wameanza kuupigia hesabu ubingwa wa UEFA ambapo watakutana na Real Madrid katika mchezo wa fainali wiki ijayo.
Kutokana na mafanikio makubwa ya Atletico msimu huu, Cerezo anaamni timu hii itaingia katika kitabu cha historia ya klabu hii na ni zawadi tosha kwa mashabiki wa klabu hiyo.
“Hii ndio ligi ambayo siku zote wanasema timu sahihi inabeba kombe,” Aliwaambia waandishi wa habari. “Hali ilitulia baada ya Barcelona kufunga bao kipindi cha kwanza, lakini nilikuwa na wasiwasi dakika 10 za mwisho”.
“Ulikuwa mchezo mzuri mno na matokeo yalivuta hisia kubwa. Hii ndio timu itakayokumbukwa milele”.
“Ushindi huu ni muhimu zaidi ya ule wa 1996, ni muda mrefu tumepita bila kubeba La LIGA”.
“Ubingwa huu ni zawadi kwa mashabiki wote wa Atletico walioteseka kwa kipindi chote na wajukuu zangu pia””
Pia rais huyo amekiri kuwepo kwa pengo la Diego Costa kama hataimarika kuivaa Real Madrid baada ya kupata maumivu ya nyama za paja hapo jana.
“Itakuwa aibu kubwa kama atakosa fainaliya UEFA kwasababu ni mchezaji muhimu mno katika timu”.

0 comments:
Post a Comment