JAMBO limezua jambo. Pamoja na kuanza kwa kishindo safari yake ya
kuelekea Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa ajili ya fainali za kuwania Tuzo za
MTV Africa (MAMA), mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na baby
wake, Wema Isaac Sepetu wamechafua hali ya hewa, Ijumaa Wikienda
lilikuwa linarandaranda ndani ya nyumba.
Pamoja na kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye shoo ya kuwatambulisha
wasanii wanaowania tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta,
Dar, Diamond hakumpandisha Wema stejini kama kawaida yake, jambo
lililozua kizaazaa.
Kuna muda mashabiki wake walipiga kelele wakimtaka Wema apande stejini lakini hakufanya hivyo.
Awali Diamond alipanda stejini mishale ya saa 8:00 akipishwa na msanii
kutoka Sauz, Jigger ambaye alikuwepo kwa ajili ya kutoa sapoti kwa
Mbongo Fleva huyo.
Msauz huyo alifanya shoo ya dakika 20 kisha akampisha Diamond ambaye
aliingia na Kibao cha Uswazi Take Away Remix, ambacho ndani yake
amemfagilia Halima Haroun ‘Kimwana’ ambaye ni hasimu wa mpenzi wake,
Wema.
Baada ya kumaliza wimbo huo ndipo baadhi ya mashabiki wakasikika wakimwambia Diamond ampandishe Wema la sivyo watakinukisha.
Ishu hiyo iliendelea hadi jamaa aliposhuka stejini hapo.
Wakati Diamond akiendelea kufanya makamuzi yake hayo, Wema na Halima
Kimwana wote walikuwepo ukumbini hapo na kwa bahati nzuri kama si mbaya
walijikuta wote wakimshangilia Diamond, tena wakiwa VIP ya juu ambapo
walikuwa wakiingia watu maalum.
Mwanahabari wetu aliwashuhudia wawili hao walipogeukiana kila mmoja alionekana kumwekea mwenzake uso wa mbuzi.
Hali hiyo ilidumu hadi Diamond alipomaliza shoo yake na Wema kushuka na kumuacha Halima Kimwana.
Baada ya shughuli za shoo Diamond alibaki na Halima Kimwana wakicheza disco.
Kufuatia hali hiyo kwenye mitandao ya kijamii usiku huohuo, kuliibuka
maneno mengi kutoka kila upande kuwa shoo ya Diamond ilichafuliwa na
Wema na Halima Kimwana ambaye alidaiwa alijipanga kwenda kumfanyia fujo
Wema kwa kuwa yupo upande wa Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata stori mbalimbali zinazowahusu mastaa kwa wakati muafaka
0 comments:
Post a Comment