IMEVUJA! Siku chache baada ya kifo cha mwongozaji na mwigizaji wa filamu
Bongo, Adam Philip Kuambiana, daktari mkubwa wa mastaa ameibuka na
kudai marehemu alijiua mwenyewe.
Kwa mujibu wa daktari huyo ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini
kutokana na maadili ya taaluma yao kuficha siri ya mgonjwa, siku moja
kabla ya kifo (Ijumaa ya Mei 16, mwaka huu), marehemu alimpigia simu na
kumwambia amekunywa dawa za malaria aina ya Fansidar lakini pia
amekunywa pombe.
ILIVYOKUWA
Daktari huyo alieleza kuwa, marehemu alimpigia simu kumuomba ushauri juu
ya nini cha kufanya na kama kuna madhara yoyote juu ya pombe hizo na
dawa alizokunywa.
“Aliniuliza kama kuna madhara yoyote ambayo anaweza kuyapata kwa kuwa
alikuwa amekunywa fansidar kwa ajili ya malaria kisha akapata kiu ya bia
na kuamua kunywa,” alisema daktari huyo.
AMSHAURI KWENDA HOSPITALI
Akizidi kuzungumzia tukio hilo, daktari alikwenda mbele kwa kusema licha
ya msanii huyo kuwa na ‘masikhala’ mara kwa mara, lakini kwa kuwa
alimwambia jambo ambalo linahusu uhai wake, alimshauri kwenda hospitali
iliyo karibu ili akaonane na daktari kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa
kutoa sumu kwani kitaalam mtu anapokunywa pombe akiwa amemeza dawa za
aina hiyo vyote hugeuka kuwa sumu.
Alisema kutokana na jinsi alivyozidi kumsimulia hali aliyonayo, aliamini
kwamba marehemu alikuwa anamaanisha alichokuwa akikisema hivyo ikabidi
amsisitize kuwahi hospitali haraka.
“Nilimwambia awahi hospitalini haraka kwani nilijua fansidar ni kali na
si dawa ya kufanyia mchezo. Lakini kesho yake nilipopata taarifa za kifo
chake niliumia sana japokuwa nilijua amejiua kwa kuchangaya fansidar na
bia maana mchanganyiko wa sumu yake mwilini ni mkali sana,” alisema
daktari huyo huku akisisitiza kusitiriwa kwa jina lake.
MAZINGIRA YA KIFO
Kwa mujibu wa mtu ambaye alikuwa karibu na Kuambiana siku ya tukio
ambaye naye hakutaka kutajwa jina gazetini, marehemu asingekufa ghafla
kama tatizo alilokuwa nalo lingekuwa la vidonda vya tumbo ambavyo
vilikuwa vikimsumbua kwa muda mrefu.
“Siku ile marehemu alikuwa na pesa, alikunywa sana pombe kutoka asubuhi
mpaka usiku mwingi, alikuwa anakula kila anapojisikia sasa hatuelewi ni
kitu gani kilitokea maana haiwezekani mtu akutwe anaendesha na kutapika
damu pasipo kuwa na sumu mwilini,” alisema mtu huyo.
DAKTARI AWAASA MASTAA
Katika hatua nyingine, daktari huyo aliwashauri mastaa wengine kuwa
makini kwani mara kadhaa amepata kesi za namna hiyo ambapo wanakunywa
pombe vilabuni usiku huku wakiwa katika dozi ya ugonjwa fulani.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali zinazowahusu wasanii
Thursday, 22 May 2014
Daktari anena na Kusema Kuambiana Amejiua !!!!!
Related Posts:
Mtanzania ateuliwa kuwa makamu mkuu wa Rais wa BET Networks. BET Networks, ambayo ipo chini ya kampuni ya Viacom Inc. imetangaza kumwajiri Kay Madati kama makamu mkuu wa rais (Executive Vice President) na pia kama Chief Digital Officer. Madati, raia wa Tanzania aliyeishi katik… Read More
Q Chilla alamba dili nonoMsanii wa muziki wa Bongofleva Abubakari Katwila almaarufu kama Q Chief amevunja ukimya kwa kupata dili la mkataba wa mamilioni na kampuni ambayo itakuwa ikisimamia kazi zake za muziki zitakazotengenezwa kwa ubora wa hali ya … Read More
Mahakama:Pistorius hakukusudia kuuaJaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp… Read More
Clouds kulishitaki gazeti la Aman kwa kumchafua Diva.Kampuni ya Clouds Media Group yenye makao makuu jijini Dar Es Salaam inataka kulishitaki gazeti la Aman kwa kumchafua mmoja wa watangazaji wake mahiri Loveness Malinzi alimaarufu kama "Diva Loveness";mtoto wa Rais wa Shirikis… Read More
Oscar hatiani kwa kuua bila kukusudiaMwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp kwa bahati mbaya Akitoa uamuzi wake jaji Thokozile Masipaal alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati … Read More
0 comments:
Post a Comment