Aliyekuwa Meneja wa Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa
Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza anazikwa leo katika Kijiji cha
Mulukulazo, Ngara mkoani Kagera huku familia yake ikisema haina cha
kusema kuhusu kifo hicho, bali inamwachia Mungu.
Akizungumza jana kijijini hapo,
mdogo wa marehemu, Alex Gashaza alisema familia imepokea msiba huo kwa
mshtuko mkubwa na kushangazwa na taarifa kwamba ulitokana na kujinyonga
kama inavyodaiwa.
Alisema baada ya kupokea simu kutoka Dar es Salaam kuhusu mazingira ya
kifo hicho, wameshindwa kujua sababu za kifo kwa kuwa hakuna mtu
aliyezungumza naye.
Alisema kaka yake hakuwa na tatizo lolote na wanafamilia, ndugu wala
jamaa zake wa karibu, hivyo familia haiwezi kuelezea jambo ambalo halina
ushahidi, badala yake inaacha tukio hilo mikononi mwa Mungu.
“Tumekuwa tukishirikiana naye kuendeleza familia yetu, kama unavyoona
nyumba ilipokuwa imefikia hatua ya kuezekwa, kuna mchango wake mkubwa
kifamilia,” alisema Alex.
Mwili wa Gashaza ulitarajiwa kuwasili Mulukulazo jana jioni na leo saa
4:00 asubuhi utapelekwa katika Kanisa la Anglikana katika kijiji hicho
kwa ajili ya sala na saa 6:00 mchana utaagwa kabla ya mazishi
yatakayofanyika nyumbani kwake.
Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza mkoani
Mwanza, Mchungaji Lazaro Manjelenga ambaye pia ni baba mkwe wa mdogo wa
marehemu, alisema wana matumaini na Muumba kwa kile kilichotokea.
“Siri ya Mungu na mwanadamu wake hakuna wa kuijua, hivyo tusihukumu,”
alisema na kuongeza kuwa mazishi yatafanyika kwa mujibu wa taratibu za
Kanisa hilo.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com hupata habari mbalimbali kama hizi kwa wakati muafaka.
Dr.John Magufuli:Ajenda ni maendeleo na si kuchagua vyama.Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amewataka Watanzania kuweka vyama vyao pembeni, badala yake kuweka mbele ajenda ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika jimbo la…Read More
Wakenya 3 wauawa kwa Ujambazi Arusha.Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas Arusha amesema Majambazi wane, wakiwemo raia watatu wa Kenya wameuwa na polisi mkoani Arusha baada ya kuhusika kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi wa kupora silaha pamoja na…Read More
Wanachama 600 na viongozi 15 wa UKAWA Jimbo la Vunjo wahamia CCM.Taarifa tuliyoipokea kutoka jimbo la Vunjo ambalo Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR MAGEUZI anagombea ubunge.
Lakini baada ya hapo jana Bantuz.com kuripoti taarifa kuhusiana na kutokea kwa mgawanyiko wa wana-UKAWA katika jimbo hil…Read More
Lowassa awaambia wananchi wa Muleba wamfungie magoli 3.Wananchi wa Jimbo la Muleba Kusini wakizungusha mikono wakiashiria kutaka mabadiliko walipokuwa kwenye Uwanja wa Fatuma, Muleba ulipofanyika mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa, mkoani Ka…Read More
0 comments:
Post a Comment