Saturday, 17 May 2014
Jipya Kuhusu Jay Z Kuwa Msimamizi Wa Kanye West Kwenye Harusi Yake
Baada ya tetesi kuwa Rapa Jay Z pamoja na mkewe Beyonce wamesusia na hawatahudhuria harusi ya Kanye West pamoja na Kim Kardashian, ripoti mpya zimeibuka kuwa mpango wa mastaa hawa kuhudhuria harusi hii upo na Jay Z mwenyewe ndiye atakayekuwa msimamizi wa Kanye katika harusi hii.
Kwa mujibu wa mtandao wa Radar Online, mastaa hawa watahudhuria harusi hii ambayo Jay Z pamoja na Beyonce wangependa kwa sehemu kubwa matukio yake yasirekodiwe kwa ajili ya kurushwa katika televisheni, bali iwe ni shughuli ya binafsi.
Taarifa hii mpya inakuja siku kadhaa baada ya Kim Kardashian kuweka wazi kuwa, hawatarekodi harusi hii kwa ajili ya kurusha katika kipindi maarufu cha uhalisia cha familia yao cha Keeping Up With The Kardashians.
0 comments:
Post a Comment