Timu ya Arsenal ya England
imetwaa kombe la FA baada ya kubamiza Hull City kwa jumla ya magoli 3 – 2
kwenye fainali iliyofanyika katika uwanja wa Wembley siku ya jumamosi.
Katika mechi hiyo ya fainali Hull City ndio
waliokuwa wa kwanza kuutikisa wavu wa Arsenal kwa magoli mawili ya
haraka haraka yaliyofungwa ndani ya dakika 10 kipindi kwanza.Hata hivyo magoli hayo hayakuweza kudumu kwani katika dakika ya 16 Santiago Cazorla aliifungia Arsenal goli na hivyo hadi mapunziko matokeo yakawa 1 – 2.
Katika kipindi cha pili Arsenal walikuja juu na kusawazisha goli hilo katika dakika ya 80 lililofungwa na Laurent Koscielny na kuwa 2 – 2 na hivyo kufanya mechi hiyo imalizike dakika 90 za kawaida kwa sare ya 2 - 2 bila kumpata bingwa.
Baadae mwamuzi wa mpambano huo Lee Probert aliongeza dakika nyingine 30 ambazo zilifanya Arsenal wajiongezee goli la tatu na la ushindi katika dakika ya 108 lililofungwa na Aaron Ramsey.
Gunners ilishinda taji lake la mwisho mwaka 2005 katika fainali za kombe la F.A ambapo iliwacharaza wapinzani wao wa jadi Manchester United katika mechi iliochezewa katika uwanja wa Cardiff,huku timu ya Hull City ikishiriki kwa mara ya kwanza katika fainali ya kombe hilo.
Meneja Arsene Wenger ameshinda mataji saba muhimu katika miaka yake 18 kama mkufunzi wa timu ya Arsenal, ikiwemo mataji matatu ya ligi kuu ya uingereza pamoja na manne ya kombe la F.A.
Mashabiki wa timu zote mbili walikabidhiwa tiketi 25,000 kila mmoja huku tiketi nyengine 20,000 zikipewa watu waliojitolea katika mashirika ya hisani,vilabu na ligi za kaunti.
0 comments:
Post a Comment