Polisi wa kupambana na ghasia
wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya maelfu ya waandamanaji
katika barabara za miji ya Sao Paolo na Rio de Janeiro walipinga mfumuko
wa gharama ya uenyeji wa kombe la dunia litakaloanza mwezi ujao nchini
Brazil.
Baadhi ya waandamanji walipura mawe na kuchoma
magurudumu ya magari na kufunga mabarabara ya miji wakidai serikali
haikuzingatia matakwa ya wananchi kama vile elimu sekta ya afya na
muundo msingi .Wengi wao waliahidi kurejea mabarabarani kadri mchuano huo unavyosongea .
Mwaka uliopita takriban watu milioni moja walishiriki maandamano wakilalamikia ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na ongezeko la gharama ya uandalizi wa kipute hicho cha fainali ya dimba la dunia .
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 12 June.
Waandamanaji walianzia Sao Paulo,karibu na uwanja wa Corinthians Itaquera karibu na mtaa wa Itaquera .
Uwanja huo wa Corithians ndio utakaoandaa mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia mwaka huu tarehe 12 juni.
Kulingana naye hangependa viwanja vilivyogharimu mabilioni ya dola viharibiwe ila wafanyikazi wanaojenga viwanja hivyo wajengewe nyumba kuambatana na ubora wa shirikisho la soka duniani FIFA.
Serikali imepinga uhisano wowote kati ya maandamano haya na kombe la dunia .
Waziri wa michezo Aldo rebelo amenukuliwa akisema kuwa ameona matakwa ya waandamanaji na ikampa matumaini maandamano hayo hayataathiri ujio wa takriban watalii milioni tatu na wageni laki sita wanaotarajiwa kuzuru miji itakayoandaa mechi za kombe la dunia.
Hata hivyo maandamano haya yanawadia wakati ambapo serikali inakabiliwa na mgomo wa wafanyikazi wa umma na hata polisi katika jimbo la Pernambuco
0 comments:
Post a Comment