Rais wa Nigeria ametupilia mbali
matakwa ya la kundi la kiislam la Boko Haram kwamba serikali iwaachilie
huru wafungwa wa kundi hilo ndipo litawachilia wasichana zaidi ya 200
waliiotekwa na kundi hilo.
Serikali ya Nigeria imesema iko tayari kwa mazungumzo na kundi la wanamgambo la Boko Haram.Kwa mujibu wa waziri wa Uingereza anayehusika na masuala ya Afrika Mark Simmonds aliye ziarani nchini Nigeria, Rais Goodluck Jonathan amemwambia wazi kuwa serikali haitakubali pendekezo la Boko Haram kubadilishana wafuasi wake waliofungwa jela na serikali na wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Lakini hilo ndio sharti pekee ambalo kiongozi wa Boko Haram , Abubacar Shekau ametoa.
Waziri huyo wa Uingereza amesema baada ya mzozo uliopo kutatuliwa kuna haja ya kuwajibisha waliotekeleza utekaji nyara huo ambao ni , Abubacar Shekau na wafuasi wa Boko Haram.
Tamko hilo pia linaongezea uzito katika msimamo wa serikali na hivyo kutilia shaka uwezekano wa mzozo huo kutatuliwa kwa haraka.
0 comments:
Post a Comment