Facebook

Saturday, 17 May 2014

MKOSI WA GUTTMAN BADO WAIANDAMA BENFICA YAPOTEZA FAINALI YA 8..




...Klabu ya Benfica ya Ureno jana usiku ilijikuta ikipoteza fainali yake ya 8 katika mashindano ya Ulaya baada ya kufungwa penati 4-2 na Sevilla ya Hispania katika fainali ya ligi ya Europa katika dimba la Juventus jijini Turin Italia.
Yawezekana huu ni mkosi wa aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo miaka ya 1960.
Muhangaria kwa jina la Bella Guttman aliiongoza Benfica kuchukua ubingwa wa Ulaya mwaka 1961 na 1962 baada ya mafanikio hayo kocha huyo aliomba kuongezewa mshahara ndipo uongozi ulipokataa na kumtimua lakini wakati anaondoka alijiapia kua Benfica hawatachukua ubingwa katika michuano hiyo kwa miaka 100.

Photo: Éxtasis, puesta en escena y espontaneidad en un Sánchez Pizjuán entregado a los campeones http://bit.ly/1gaqjP8 
 Tangu alipoondoka Benfica imefika fainali mara 8 na haijafanikiwa kuchukua na hii ni fainali yake ya pili kwa miaka ya hivi karibuni inapoteza ikumbukwe mwaka jana walipoteza pia katika fainali walipofungwa na Chelsea ya England.

0 comments:

Post a Comment