Facebook

Saturday, 17 May 2014

Park Ji Sung atangaza kustaafu soka....

 
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Man united na timu ya taifa ya Korea Park Ji Sung amestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 33 na hii inatokana na majeruhi ya mara kwa mara ya goti yanayomwandama.
Park aliyeichezea nchi yake ya Taifa mechi 100 amemalizia soka lake akiwa PSV Eindhoven ya Uholanzi klabu iliyomtoa katika soka la mataifa.
Baada ya kuifikisha PSV fainali ya ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2004/2005 chini ya kocha Guus Hiddink ndipo Sir Alex Ferguson alipomsajili kwa ada ya uhamisho paund milion 4.
Akiwa Old trafford Park Ji-Sung alicheza mechi 205 na kufunga magoli 27 kabla ya kujiunga na QPR mwaka 2012 ambapo alicheza mechi 20 kabla ya timu hiyo kushuka daraja na Park kupelekwa PSV kwa mkopo msimu uliopita.
Huyu ndo Park Ji-Sung. Unamkumbuka kwa lipi huyu jamaa?Tupia comment yako hapa chini !!!

0 comments:

Post a Comment