Ubalozi wa Saudi Arabia umefunga ofisi zake mjini Tripoli
kutokana na otovu wa usalama nchini Libya.
Balozi Mohammed Mahmoud al-Ali amesema kuwa wafanyakazi wote wa ofisi yake
wameondoka nchini humo kutokana na hali mbaya ya usalamaViongozi wa Libya wamekumwba na wakatai mgumu kujaribu kurejesha utulivu nchini humo tangu Muammar Gaddafi kuondolewa mamlakani mwaka 2011 na kuuawa .
Wakati huohuo, mkuu wa jeshi la Libya, ameamuru kupelekwa kwa wapiganaji watiifu kwa serikali mjini Tripoli siku moja baada ya watu waliokuwa wamejihami kujaribu kuvamia bunge la taifa.
Mapigano zaidi yameripotiwa kutokea kati ya wapignaji kutoka makundi hasimu huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu makabiliano zaidi kuzuka.
Wanajeshi katika kambi moja ya jeshi katika mji wa Tobruk, wameripotiwa kujiunga na kikosi cha wanajeshi waasi kinachoongozwa na jenerali muasi ambaye serikali inasema amekuwa akijaribu kupindua serikali.
Khalifa Hiftar aliongoza kusema kuwa mashambulizi dhidi ya wapiganaji waisilamu mjini Bengazhi yalifanyika siku ya Ijumaa. Watu sabini waliripotiwa kufariki.
0 comments:
Post a Comment