Friday, 2 May 2014
Sheikh Ponda azidi kusota rumande......!!!
Kesi inayomkabili kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda imeendelea kupigwa kalenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro.
Ilielezwa mahakamani hapo jana kuwa kesi hiyo haiwezi kusikilizwa kwa sasa kwa kuwa jalada lake bado halijarudi kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kutotii amri halali ya iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, kutoa maneno yenye kuharibu imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa, makosa ambayo anadaiwa kuyatenda Agosti 10 mwaka jana katika eneo la Uwanja wa Ndege Manispaa ya Morogoro.
Baada ya kutajwa kwa kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mary Moyo alisema kesi hiyo itaendelea kutajwa mpaka jalada hilo lililoitishwa Mahakama Kuu Oktoba 15 litakaporudishwa Mahakama ya Morogoro.
Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo jana chini ya ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na sihala za moto, mabomu ya machozi na mbwa huku wafuasi wake wakizuiwa nje ya uzito wa mahakama hiyo.
Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Lilian Lutabula aliyeshirikiana na mwendesha mashtaka wa polisi, Zabron Msusi wakati upande wa utetezi uliwakilishwa na wakili Josephine Jackson kwa niaba ya wakili Bathoromeo Tarimu anayemtetea Sheikh Ponda.
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mshtakiwa Ponda alirudishwa rumande ambako ataendelea kupafanya kuwa maskani yake hadi Mei 5 mwaka huu kesi hiyo itakapoendelea kutajwa mahakamani hap
Related Posts:
Wenje: Uchumi wa Tanzania unakua kwenye makaratasi na mifuko ya watawala "Amesema ni muhimu mjadala huo wa kitaifa kwakua hali mbaya sana kiuchumi,misamaha ya kodi imekua mikubwa,wakubwahawalipi kodi wakati wauza vitumbua wanalipa kodi,uchumi unakua kwenye mifuko ya watawala.Hivyo tuwe na m… Read More
Zanzibar yazidi kuchafuka,Bomu lalipuka karibu na msikiti na kuua Mtu 1 amefariki na wengine kujeruhiwa baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa bomu, kurushwa karibu na msikiti, darajani Zanzibar. Kuna taarifa ya kutokea mlipuko na mlio mkubwa mithili ya bomu umetokea mae… Read More
Maajabu yaonekana.Baada ya Soko la Karume Kuungua Hiki ni kitu ambacho kilipatikana mara baada ya moto kuzimwa eneo hilo la soko,Kila mtu ana maswali mengiiiiii bila majibu Je ni kitu gani hicho?au wewe ndugu msomaji unaweza tambua ni kitu gani Hiki? … Read More
Bibi kizee mchawi adondoka kutoka angani huko Jijini Mwanza. Kila mtu alikuwa na lake kuhusu bibi huyu anayedaiwa kukutwa akiwa uchi huku wengine wakisema ni mgonjwa wa akili na wengine wakidai ni mchawi kaanguka na ungo. Alipokuwa akihojiwa amedai ametoka Bariadi lakini we… Read More
Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2014/2015. Kama ilikupita hii ndiyo hotuba waweza kuisoma hapa kwani ni jukumu lako kupata habari na kuhabarishwa kila kitakachokuwa kinatufikia kwa wakati na muda muafaka.Bajeti hiiimesomwa na Mheshimiwa Mbunge Saad… Read More
0 comments:
Post a Comment