Rais wa Sudan kusini Salva Kirr
ameonya kuwa taifa lake linakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kufuatia
vita vikali vinavyoendelea nchini humo.
Tayari serikali ya Norway inaandaa kongamano la kimataifa kuchangisha fedha za kuisaidia nchi hiyo.Wiki iliopita Rais Kiir aliahirisha uchaguzi wa urais uliotarajiwa kufanyika mwezi ujao ili kutoa fursa kwa mazungumzo ya amani kati ya serikali yake na waasi.
Zaidi ya watu milioni moja wametoroka makao yao tangu vita vizuke nchini humo.
Vita hivyo viluzuka mwezi Disemba baada ya rais kudai kuwa bwana Machar alikuwa anapanga njama za kuipindua serikali yake-madai ambayo bwana Machar amekana.
Bwana Kiir amemshutumu aliyekuwa makamu wa rais Machar kwa kuchochea uhasama wa kikabila kati ya watu wa kabila la Nuer na Dinka na pia kukiuka mkataba wa kusitisha mapigano uliotiwa saini mjini Addis Ababa mapema mwezi huu
Umoja wa Mataifa umetuhumu pande zote husika katika vita hivyo kwa kutenda uhalifu dhidi ya bindamau ikiwemo mauaji na ubakaji na hata kutishia kuwawekea vuikwao ikiwa hawatasitisha vita.
0 comments:
Post a Comment