Kundi la al-Shabab limewakamata wanawake takriban 100 na kuwataka kuvaa nguo kwa mujibu wa dini ya Kiislam, vinginevyo watapigwa mikwaju.
Wanawake hao walikamatwa katika mji wa Buale, karibu kilomita 300 kusini mashariki mwa mji mkuu Mogadishu.
Mchambuzi wa masuala ya Somalia Mohamed Mohamed amesema ni mara chache sana al-Shabab hukamata watu wengi kiasi hicho.
Al-Shabab hudhibiti maeneo ya kusini na kati mwa nchi.
Wanawake hao walikamatwa wakiwa sokoni na kupewa onyo kabla ya kuachiliwa.
Kwa sababu lilikuwa kosa lao la kwanza, hawakupewa adhabu yoyote, lakini watachapwa bakora iwapo watakamatwa tena.
Hata hivyo wanawake wengi nchini Somalia huvaa niqab hata nje ya maeneo yanayodhibitiwa na al-Shabab.
Hivi sasa
tunahamia katika site yetu mpya inayoitwa www.bantutz.com
ni katika kuboresha huduma zetu za kutoa habari za uhakika na burudani.
0 comments:
Post a Comment