Kocha Arsene Wenger yuko kwenye mbio za kumuwania Mario Balotelli.Timu ya AC Milan wako mbioni kutua mzigo huo wa zamani wa Manchester City kwenye kipindi hiki cha jua, Arsenal wameshapaza sauti.
Meneja wa washika bunduki amekuwa akimhusudu Balotelli (23), pamoja na kwamba ana matatizo ya kinidhamu hasa wakati alipokuwa City ambapo alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakiipamba Ligi Kuu.
Balotelli, ambaye aliifungia AC Milan magoli 30 katika mechi 54, ana umuhimu wa kurejea Uingereza baada ya kuwa mchezaji wa ziada kwa wachezaji wa San Siro.
Nguli hao wa Italia wanataka pesa taslimu kwa ajili yake na kukata malipo yao ya posho baada ya kumsainisha kwa pauni milioni 24 miezi 18 iliyopita.
Wenger alijaribu kumsainisha Balotelli kabla ya kwenda City akitokea Inter Milan na alizungumza naye mwaka 2009 kuwa ana uwezo wa kufika mbali.
Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi
0 comments:
Post a Comment