Manchester United imekwisha fahamu wachezaji watano inayowataka, na meneja mpya Louis van Gaal atapewa paundi milioni 220 kuwapata. Van Gaal anataka kumchukua kiungo Kevin Strootman kutoka Roma ya Italia (Daily Express),
Frank Lampard ameambiwa hatopewa mkataba mpya na Chelsea, na
huenda akaenda kucheza Marekani (Mail on Sunday),
Liverpool itasitisha
mazungumzo ya mkataba mpya na Raheem Sterling baada ya winga huyo kudai
mshahara wa paundi laki moja kwa wiki (Sunday Mirror),
Beki wa Arsenal,
Bacary Sagna amekataa dau kubwa zaidi kutoka Dubai na Monaco, na
kukubali mshahara wa laki moja na nusu kwa wiki atakaopewa na mabingwa
wa EPL, Manchester City (Sun),
Roma wamewaambia Chelsea na Tottenham
kuwa watalazimika kutoa si chini ya paundi milioni 50 kama wanamtaka
Mehdi Benatia (Metro),
Southampton wameweka dau la paundi milioni 30 kwa
kila mmoja- Luke Shaw na Adam Lallana. Shaw ananyatiwa na Man United na
Liverpool wanamtaka Lallana, na wapo tayari kutoa paundi milioni 25
(Daily Express),
Harry Redknapp wa QPR anataka kumsajili beki wa
Liverpool Glen Johnson (Daily Star),
Everton wanataka kuongeza mshahara
wa James McCarthy mara dufu ili asiondoke. Mchezaji huyo kutoka Ireland
ananyatiwa na Man United (Daily Star),
Striker wa Liverpool Luis Suarez
atapata ugumu kusema "hapana" iwapo Real Madrid watamtaka, hiyo ni kwa
mujibu wa wakili wake (Independent),
kipa wa Man U, David de Gea
ameitaka klabu yake kumsajili Andres Iniesta kutoka Barcelona
(Independent),
Barcelona wamesema Cesc Fabregas atapatikana kwa paundi
milioni 30. Man United imeacha kumfuatilia, lakini Chelsea, Arsenal na
Man City zinamtazama (Daily Telegraph),
Man United inaonekana kuzidiwa
kete na Barcelona katika kumsajili beki kutoka Ujerumani Marquinhos
anayechezea PSG (Daily Express),
Man City, Arsenal na Man United
zinamfuatilia Xavi wa Barcelona (Daily Star),
Arsenal kuanza mazungumzo
na Real Madrid kuhusu Karim Benzima na Alvaro Morata (Daily Express),
Arsenal pia wanataka kumsajili kipa wa Nice ya Ufaransa, David Ospina
(RMC),
Liverpool inajiandaa kumsajili kiungo wa Valencia Seydou Keita
(Daily Express),
Southampton inataka kumsajili beki Neil Taylor kuchukua
nafasi ya Luke Shaw (Daily Express),
Bayern Munich imekamilisha
usajili wa Ezequiel Garay kutoka Benfica (Clarin),
NA HATIMAYE.. beki wa
Real Madrid Sergio Ramos amechora tattoo ya Kombe la Champions League
kwenye kiwiko cha mguu wa kushoto. Ana tattoo ya Kombe la Dunia kwenye
sehemu kama hiyo kwenye mguu wake wa kulia.

Share tetesi hizi na wapenda
soka wote. Tetesi nyingine kesho panapo majaaliwa.
Tuko
katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma
zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi
0 comments:
Post a Comment