Facebook

Wednesday, 4 June 2014

Beckham kurejea uwanjani hivi karibuni..


Aliyekuwa mchezaji wa Uingereza na Manchester United David Beckham amedokeza kuwa huenda akarejea uwanjani akiichezea timu yake inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS Major League Soccer huko Miami.
Nahodha huyo wa zamani wa Uingereza 39 alistaafu mwezi Mei 2013 baada ya kucheza kwa miaka 20 iliyokamilikia Paris St-Germain.
 Beckham alisema hakujawahi kuwa na mchezaji mmiliki lakini haoni kwanini kusiwe naye.

Beckham

"1992-2003: Manchester United 1994-1995: Preston North End 2003-2007: Real Madrid 2007-2012: Los Angeles Galaxy 2009-2010: AC Milan 2013: Paris St-Germain  2010: Uingereza"
Kipindi hicho kinamwangazia nyota huyo wa Uingereza akisafiri maili 800 kwa pikipiki ngalawa na kwa ndege kuelekea kwenye msitu mkubwa zaidi wa Amazon Marekani ya kusini katika ziara ya siku 12.
Beckham anasema kuwa amepumzika vya kutosha na kuwa anapania kurejea uwanjani siku moja ,akijiuliza baada ya kutizama mechi za mpira wa vikapu iwapo anaweza kurejelea hali ya ushindani hata baada ya kustaafu.
Aliwahi kuichezea Uingereza katika mechi 115.
Katika kandarasi yake alipokuwa akiichezea timu ya Los Angeles Galaxy Beckham alitia sahihi kipengee kinachomruhusu kununua timu moja katika ligi hiyo kwa pauni milioni £25m na sasa anaazimia kuzindua klabu huko Miami katika msimu wa 2016 ama 2017.

 Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.

Related Posts:

  • Man City yamuwekea dau Alex SongManchester City imeonyesha nia ya kupata huduma ya mchezaji wa Barca Alex Song ambaye msimu huu alikuwa akicheza kwa mkopo timu ya Westham inayoshiriki.Alex aliyerudi nyumbani Barcelona anaweza kuuuzwa jumla na kujiunga na … Read More
  • Dante atakiwa Man United.Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Dante anatakiwa na timu ya Manchester United kwenda Old Trafford msimu huu. Timu ya Manchester ipo tayari kumpa mkataba mchezaji huyo kujiunga na mashetani hao.Lakini mchezaji mwenyewe Dante am… Read More
  • Skrtel akataa kusaini kataba mpya Liverpool.  Beki wa klabu ya Liverpool Martin Skrtel amefichua kuwa bado hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo kama ambavyo inaripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini England pamoja na nyumbani kwao huko Slovakia. Skr… Read More
  • Juventus yamnasa mshambuliaji hatari Paulo Dybala Mabingwa wa ligi kuu ya Italia Juventus leo hii wamethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji Paulo Dybala kutoka katika klabu ya Palermo kwa kitita cha euro milioni 32. Mshambuliaji huyo mwenye umri … Read More
  • Benitez amtaka Laurent KoscielnyKocha mpya wa Real Madrid Benitez anataka kumsaini beki wa Arsenal Laurent Koscielny. Ni imani ya kocha wa zamani wa Liverpool na Chelsea atampata Mfaransa huyo kuwa msaidizi wa Sergio Ramos katika ulinzi. Koscielny alisai… Read More

0 comments:

Post a Comment