Facebook

Friday, 20 June 2014

FIFA kuchunguza Mexico kwa ubaguzi


Shirikisho la kandanda Duniani FIFA limeanza kuchunguza hatua ya kuiadhibu Mexico, baada ya madai kujitokeza kuwa mashabiki wake walihusika katika matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi yao na Cameroon.
Katika taarifa, FIFA imesema kuwa uchunguzi huo umeanzishwa baada ya matamshi kutolewa kuwa mashabiki wa Mexico walionyesha vitendo na matamshi ya kutiliwa shaka.
Aidha duru kutoka FIFA zimeiambia BBC kuwa wanachunguza ripoti ya matamshi machafu kutoka kwa mashabiki wa timu ya Brazil pamoja na mabango ya kibaguzi wakati wa mechi kati ya Croatia na Russia.
Mwaka jana FIFA ilibuni sheria kali ambapo matamshi ya kibaguzi kutoka kwa shabiki wa soka au mchezaji, yanaweza kuchochea adhabu kali hata kulazimisha timu husika kucheza mechi bila ya mashabiki, kunyanganywa alama, kushushwa daraja au hata kufukuzwa kushiriki mchuano.

Related Posts:

  • MAYWEATHER KUZICHAPA TENA NA MAIDANA Floyd Mayweather ametangaza kuwa atapanda ulingoni kupambana na Marcos Maidana, Septemba 3 mwaka huu mjini Las Vegas. Mayweather alimzidi Maidana katika mpambano uliozua utata mwezi Mei, na alisema kuwa atarudiana na … Read More
  • FIFA yazuia Suarez kutambulishwa Barcelona.   Fifa imezuia mipango ya Barcelona kumtambulisha rasmi Luis Suarez mbele ya mashabiki kwenye dimba la Nou Camp. Fifa imesema adhabu aliyopewa haimruhusu kujihusisha na shughuli zozote za soka. Mwaka jana Neyma… Read More
  • FIFA YATANGAZA WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA Fifa imetangaza orodha ya majina 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora katika michuano ya Kombe la Dunia - 2014 Golden Ball. Wachezaji watatu wametoka Argentina, Angel Di Maria, Javier Mascherano na Lionel Messi. Maha… Read More
  • Tiketi za Manchester United zashambuliwa kwa nguvu.   MANCHESTER UNITED imetangaza kuwa Tiketi zote 55,000 za kuingia kwenye Mechi Uwanjani Old Trafford kwa Msimu mzima zimeuzwa na hii imevunja Rekodi ya Tiketi za Msimu kumalizika mapema. Wachambuzi wanadai kuu… Read More
  • David Rudisha azidi kung'ara Olimpiki.   David Rudisha ameshinda mbio za mita 800 wanaume katika mbio za Diamond League za Scotland. Mara ya mwisho kuwa nchini Uingereza Rudisha alishinda medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki ya London 2012. Mwa… Read More

0 comments:

Post a Comment