Facebook

Saturday, 21 June 2014

Idadi ya wakimbizi yaongezeka duniani

Wakimbizi wengi wametokana na vita vinavyoendelea nchini Syria
Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, linasema idadi ya watu waliopoteza makao yao na kufanywa wakimbizi kutokana na vita ilizidi milioni hamsini mwaka jana.
Idadi hii inasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya dunia.
Takriban watu milioni 17 walitoroka nchi zao na zaidi ya milioni thelathini ni wakimbizi wa ndani ya nchi zao.
Wengi wameishi katika kambi za wakimbizi kwa miaka mingi.
Vita nchini Syria, ni moja ya sababu kuu ya kuongezeka kwa idadi hiyo ya wakimbizi, lakini pia kuna mizozo mingine katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na nchini Sudan Kusini ambayo imechangia idadi kubwa ya wakimbizi
Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, linasema kuwa idadi hiyo ni ishara tosha ya athari za kukosa kuzuia mizozo. Pia limesema kuwa mataifa tajiri yanapaswa kufanya juhudi kuhifadhi wakimbizi hao.

Related Posts:

  • Boko Haram wazuia watu kuzika maiti Wapiganaji wa Boko Haram wamesababisha maafa Kaskazini ya Nigeria ngome yao ya vita Taarifa za kutisha zimeibuka kutoka mjini Bama moja… Read More
  • KESI YA KENYATTA YAPIGWA KALENDAWaendesha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC iliyopo The Hague wameomba kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuahirishwa tena. Bwana Kenyatta anashtakiwa kwa makosa dhidi ya ubinaadam, lakini upande wa mashtaka umes… Read More
  • HATIMAYE KIONGOZI WA AL SHABAB AUAWA Aliyekua kiongozi mkuu wa Alshabab Ahmed Abdi Godane ameripotiwa kuuawa!! Habari kutoka katika idara kuu ya ulinzi ya marekani PENTAGONI imesema kua kuuawa kwa kiongozi huyo mwanzilishi wa kikundi ambacho kimekua mwiba mkali… Read More
  • Al-Qaeda yafungua tawi jipya India Kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri amesema kuwa wamefungua tawi jipya la mtandao huo wa kigaidi nchini India i… Read More
  • Mafuriko yaua nchini India Watu kadhaa wanahofiwa kufa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuchukuliwa na maji katika jimbo la Kashmir nchini India. Basi hilo … Read More

0 comments:

Post a Comment