Watu zaidi ta arobaini na tano wameuawa katika mashambulizi ya Mpeketoni
Kundi la wapiganaji wa Al
Shabaab nchini Somalia, limekiri kufanya mashambulizi katika eneo la
Mpeketoni karibu na Lamu, Pwani ya Kenya.
Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya watu 49.Taarifa ya kundi hilo ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi dhidi ya serikali ya Kenya kwa kufanya msako dhidi ya waisilamu kwa njia ya kuwafunga kiholela na kuwaua wahubiri wa kiisilamu.
Baadhi ya walioshuhudia mashambulizi hayo wamearifu kuwa wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi japo Polisi hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.
Mji wa Mpeketoni uko umbali wa kilomita mia moja kutoka eneo la mpakani na Somalia.
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment